Jumapili , 27th Jun , 2021

Mnamo Juni 27, 1967, Automated Teller Machine (ATM) ilianza kutumika na inaelezwa kuwa mwigizaji Reg Varney ndiye mtu wa kwanza kutoa fedha kwa kutumia mashine hiyo inayojiendesha katika mji wa Enfield, kaskazini mwa Uingereza.

Mteja akitumia ATM

ATM ya kwanza ilianzishwa na mvumbuzi wa Uingereza anayeitwa John Shepherd-Barron na inatajwa kuwa mashine iliruhusu wateja kutoa kiwango cha juu cha GBP10 kwa wakati mmoja.