Alhamisi , 29th Sep , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara imekutana na kampuni 27 za nchini Italia ambazo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, utalii na Nishati.

Balozi wa Italy Tanzania Marco Lombardi

Katika kikao Cha pamoja na viongozi wa makampuni hayo ambao wakingozwa na Balozi wa Italy Tanzania Marco Lombard serikali imewahakikishia biashara yenye mazingira ya utulivu kwneye uwekezaji.
 
Hata hivyo Balozi wa Tanzania nchini Italy mahoomud Thabit Kombo historia kati ya Tanzania na Italia ni nzuri katika viwanda hivyo Diplomasia ya Uchumi Kwa sasa inajitangaza.

"Diplomasia yetu ya Uchumi ambayo Tanzania imejipambanua nayo kimataifa inazidi kuleta wawekezaji kwenye sekta mbalimbali Kila kukicha hivyo ni vyema sasa kuzitazama fursa hizo kukuza mitaji na pato"alisema Mahamoud Thabit Kombo-Balozi wa Tanzania nchini Italy.