Jumatano , 22nd Sep , 2021

Teknolojia inaenda kasi sana kwasasa, na makampuni mbalimbali haijawaacha nyuma baada ya kampuni  ya Klein Vision ikishirikiana na Hyundai na BMW zimeunda gari “AirCar OM-KLZ" inayopaa angani.

Picha ya Gari (AirCar OM-KLZ) ikiwa angani

 Gari hiyo imefanikiwa katika majaribio siku za hivi karibuni kwa kupaa kwa dakika 35 na kutua salama uwanja wa ndege wa Nitra na Bratislava nchini Slovakia huku ikiwa na uwezo wa kupaa kwa Kilomita 1,000 kwa speed ya 170km/h bila kutua, kwa urefu wa futi 8,2000 kutoka usawa wa bahari. 


Inaweza kufungua mabawa, kurefusha mkia na kubadilika kuwa kama ndege kwa sekunde 15,imetumika injini ya BMW yenye nguvu ya 160HP na kuunganishwa na propeller nyuma ya gari na linatumia mafuta na mfumo wa petrol kama gari za kawaida huku ikiwa na uwezo wa kubeba watu wawili na uzito usiozidi kilo 200.